Monday, 9 January 2017
John Terry: Chelsea yapanga kukata rufaa kadi nyekundu
Jurgen Klopp: Sikukosea kuchagua kikosi cha Liverpool FA
Tuesday, 3 January 2017
Guardiola: Nakaribia kustaafu kufundisha soka.
Image captionGuardiola amezifundisha klabu za Barcelona na Bayern Munich kwa mafanikio makubwa
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anakaribia kustaafu kufundisha soka na hataitakuwa miaka 65 kama alivyodhani awali.
Muispania huyo amewahi kuifundisha klabu ya Barcelona ka mafanikio makubwa kisha Bayern Munich kabla ya kuchukua nafasi ya Manuel Pellegrini Man city.
''Nitakuwa hapa Manchester kwa misimu ama mitatu labda na zaidi,'' Guardiola mwenye miaka 45 alisema kabla ya ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Burnley.
''Sitakaa kwenye benchi mpaka miaka 60-65.Nafikiri mchakato wa kuanza kusema kwaheri umekaribia.
Guardiola ameshinda vikombe 14 katika miaka minne akiwa na Barcelona, ikiwa ni pamoja na vikombe vitatu vya La Liga na viwili vya ligi ya mabingwa Ulaya.
Alipumzika mwaka mzima kabla ya kujiunga na Bayern Munich na kuwaongoza kupata vikombe vitatu vya ligi kuu licha ya kukosa ligi ya mabingwa Ulaya
Kikosi cha Guardiola kilicheza pungufu baada ya Fernandinho kupewa kadi nyekundu lakini magoli ya Gael Clichy na Sergio Aguero yaliwapa ushindi.
Wafungwa 55 wapoteza maisha Brazil.
Maafisa nchini Brazil wanasema wafungwa 55 wamepoteza maisha katika vurugu zilizotokea katika gereza nje ya mji wa Manaus.
Vurugu hizo katika gereza la Anisio Jobim zilianza siku ya Jumapili na kuisha baada ya saa kumi na saba pindi wafungwa hao waliposalimu amri.
Baadhi ya miili imekatwa vichwa huku mingine ikiwa imechomwa moto.
Mkuu wa usalama katika jimbo la Amazonas, Sergio Fontes, amewaambia waandishi wa habari kuwa vurugu hizo zilikuwa zimepangwa muda mrefu.
"kila kitu kinaashiria kwamba vurugu zilizotokea zilikuwa zimepangwa muda mrefu.
Image captionIdadi kubwa ya wafungwa waliotoroka walikamatwa
Wafungwa waliweka bayana kwa uongozi wa gereza kwamba kila kitu kitakuwa sawa katika msimu huu wa sikukuu.
Hawakutekeleza ahadi yao, lakini huwezi kuwaamini wahalifu?"
Fontes ameongeza kusema kuwa baadhi ya wafungwa walitoroka na wengine wameuawa.
Hata hivyo, Idadi kubwa ya wafungwa waliokuwa wametoroka tayari wamekamatwa.
Nako nje ya gereza, ndugu wa wafungwa waliokusanyika walijawa na shauku ya kutaka kujua hali ya ndugu zao.
Mama wa mmoja ambae mwanae ni mfungwa ameonekana akishikilia gamba la risasi huku akisema polisi hawana nia ya kuwalinda wafungwa.
Maafisa wa gereza wanasema makundi hasimu yaliyopo nje na ndani ya gereza yamepigana kwa kutaka kuwa na sauti dhidi ya kundi jingine.
Image captionNdugu na jamaa wakiomboleza nje ya gereza
Wajumbe wa moja wapo ya makundi hayo, wametengwa katika magereza mengine.
Nae waziri wa katiba amekwenda katika gereza hilo ili kuangalia uwezekano wa kuhamishwa kwa baadhi ya wafungwa katika gereza jengine.
Jinsi ya kupika keki.
Siku zote mtu anatakiwa awe mbunifu kwa kila kitu.Ila leo nagusia upande wa jikoni.Kwa upande wa wanawake katika sekta nzima ya maakuli mambo ya jikoni shuti unatakiwa uwe mtundu,leo unabuni hiki na kesho unafanya vile ili mradi uweze kupata vionyo tofauti tofauti.Raha ya chakula shuti upike mwenyewe bibi..'mwanamke jiko eeh''.Kwa wale wanawake wafanyakazi,siku ukiwa nyumbani umejipumzisha na laazizi wako unaamua umuandalie kitu tofauti ambacho kitamfrahisha nae aone kuwa mama watoto wake anajua kulikalia jiko na si kila siku anakula chakula alichopikiwa na 'house gal'..
Leo tutaangalia namna ya kupika keki ya kawaida hasa ukiwa nyumbani.
Mahitaji:
•Unga wa ngano
•Mayai 6
•Sukari
•Baking powder vijiko 2 vya chai
•Unga wa mdalasini kijiko 1 cha chai
•Zabibu kavu
•Maziwa fresh 1/2 glasi na mtindi 1/2 glasi
•Cocoa au kahawa
•Vanilatui la nazi zito kabisa,
•Mafuta 1/4 lt
•Tray ya kuokea keki yako Sufuria/chombo cha kuchanganyia mchanganyiko wako
Hatua za kupika:
•Tayarisha oven yako kwa kuiwasha katika moto wa nyuzi 185 sentigrade (365F).
•Paka mafuta kiasi kwenye kikaangio/tray yako kisha kiweke pembeni.
•Pasua mayai yako kisha yaweke tkt 'brenda',weka sukari yako kisha washa mashine yako ili vichanganyike kwa pamoja hadi viwe laini kabisa.
•Weka unga wako ktk sefuria ,weka baking powder,zabibu,mdalasini,cocoa au unga wa kahawa,tui la nazi,maziwa fresh,mtindi,mafuta,vanilla,vichanganye alafu mwisho mimina mchanganyiko wako wa mayai na sukari kisha vichanganye vyote kwa pamoja hadi mchanganyiko wako uwe laini kabisa yaani uwe saizi ya kumiminika km uji.
•Chukua mchanganyiko wako huo alafu uumimine katika tray yako uliyoipakaa mafuta, ulioiandaa kwa ajili ya kuokea keki yako.
•Kisha uweke ktk oven kwa muda wa dk 40-45 kupika keki yako.
•Tumia toothpick au kijiti cha mbao kisafi kuchomeka katikati ya keki yako kuangalia kama imeiva vyema, baada ya hizo dakika hapo juu kupita iwapo kijiti cha mbao/ toothpick kitatoka bila ya ungaunga basi keki yako imeiva vyema, iepue na uzime jiko iwapo kijiti cha mbao/ toothpick kitatoka na unga unga basi ujue bado keki yako haijaiva vyema.
•Funga mlango na uache iive kwa muda.
•Hakikisha kijiti kinatoka bila ya unga ungaIache keki yako ipoe kwa dakika 15 - 20 kabla hujaiondoa kwenye kikaangioKeki yako ipo tayari kwa kuliwa.
Thursday, 29 December 2016
Mbinu 10 za kufaulu Mitihani.
Mwanafunzi ambaye anataka kupata alama za juu katika mtihani wake lazima awe mtu wa kujiandaa kila siku kwa kutumia dondoo zifuatazo ili kujihakikishia uwezo wa kufaulu na kuepukana na dhana ya kuishi kwa kutegemea bahati.
KWANZA: Kama nilivyosema hapo juu jambo la kwanza ni kuzingatia muda, si vema kukurupuka na kukimbizana nao na kujinyima usingizi wakati ratiba ya mtihani ilikuwa inafahamika na muhusika alikuwa na uwezo wa kujiandaa taratibu kuelekea kwenye siku ya kutahiniwa kwake.
PILI: Jindae mwenyewe kwa kutafuta na kufanya mitihani iliyopita, huku ukinakili maswali ambayo watunzi wamekuwa wakiyarudia rudia kila mwaka.
Njia hii itakuwezesha kujiandaa kwa kuzingatia shabaha na mahitaji halisi ya maswali yatokayo mara nyingi kwenye mitihani. Hakikisha unapata mitihani ya nyuma ya ngazi uliyopo isiyopungua kumi au zaidi na uifanye huku ukihakikisha hakuna swali hata moja ambalo linakushinda.
Pamoja na ukweli kwamba ubahatishaji wa vitu si njia sahihi sana, lakini umeonekana kuwasaidia wale ambao ubahatishaji wao huambatana na umakini, hivyo mwanafunzi anatakiwa kuwa na tabia ya kubahatisha maswali ambayo anadhani mwalimu wake anaweza kuyatoa kutoka kwenye daftari lake na hivyo kujiandaa.
Ubaharishaji huu, lazima uambane na kile nilichosema awali, yaani kuwa na kumbukumbu ya mitihani iliyopita. Wanasema watalaamu kuwa ulimwengu una tabia ya kurudia matukio, hivyo hata kwenye maswali kuna tabia hii ya kujirudia rudia.
TATU: Orodhesha maeneo yote ambayo huyaelewi kwenye mtihani hiyo ya nyuma na uyafanyie mazoezi kwa kupata ushauri kwa waalimu wako. Kama kuna mada ambazo hujazielewa kwenye daftari lako hakikisha muda uliojiwekea utatosha kuzielewa.
NNE: Hakikisha unajizoeza kufanya mitihani ya majaribio mara kwa mara, ambayo utaifanya kwa kuzingatia muda na masharti yote ambayo hutolewa siku ya kufanya mtihani halisi.
Haifai mwanafunzi kukimbia majaribio yanayotolewa darasani na mwalimu wake, kwani hayo ndiyo yatamuwezesha kufahamu kama amekamilika kwa kutahiniwa au bado kuna eneo linamtatiza.
TANO: Hakikisha kuwa kumbukumbu zako kichwani zinaongezeka kadiri unavyojifunza, usiwe mtu wa kusahau sahau uliyojifunza na ikiwezekana eneo ambalo unaonekana kulisahau ndilo ulipe kipaumbele cha kujikumbusha, ikibidi hata kila siku.
SITA: Angalia kwa makini alama zako za mitihani ya majaribio, ikiwa unapata alama za chini ujue kuna mahali panahitaji nguvu za ziada, shauriana na mwalimu wako maeneo yote unayokosa au yanayokusumbua kabla ya siku ya mtihani.
SABA: Ili mwanafunzi awe na uhakika wa kufanya vema mtihani wake anatakiwa kuzingatia dondoo zote zilizotolewa kwenye kipengele cha kuimarisha kumbukumbu kichwani, ambazo zimo ndani ya kitabu hiki.
NANE: Wakati mwingine ni vema ukausikiliza mwili, si vema kuulazimisha kusoma hata kama unaona kuna udhaifu:
baadhi ya wanafunzi hukesha wiki mbili mfululizo wakisoma, matokeo yake mwili na akili huchoka na kushindwa kupokea masomo vizuri. Muda wa kupumzika unahitajika.
TISA: Kabla mwanafunzi hajaingia katika chumba cha mtihani anatakiwa kujiamini kwa kushinda hofu:
Eneo hili ni muhimu sana kwani kuna wanafunzi hufeli si kwa sababu hawakujiandaa, bali hukumbwa na hofu muda mfupi kabla ya kuanza mtihani.
Hivyo ni muhimu mwanafunzi akaandaliwa kisaikolojia na waalimu pamoja na wazazi wake jinsi atakavyoweza kufanya mtihani bila hofu.
KUMI: Imani ni hitimisho la mafanikio ya mwanafunzi:
haifai kuingia katika chumba cha mtihani ukiwa na mawazo hasi.
Kinachotakiwa ni ari ya ushindi au kwa lugha nyingine ni mawazo chanya. “LAZIMA NIFAULU MTIHANI HUU” Imani hii inaweza kujengwa na mtu kupitia kujiamini mwenyewe au kuamini kwa msaada wa nguvu za imani yake ya dini.
Kama unatabia hizi 10 basi tayari wewe ni Mjasiriamali.
Kwa muda mrefu kumekuwa na mjadala mkubwa ikiwa mjasiriamali anazaliwa au anatengenezwa. Kwa kuangalia tabia za wajasiriamali na tabia za binadamu kwa ujumla, wajasiriamali wana tabia za kipekee. Wajasiriamali wanafikiri tofauti na wanatenda tofauti na watu wengine kwenye jamii.
Tabia za kipekee zinazooneshwa na wajasiriamali kuna ambao wamezaliwa nazo na kuna ambao wamezipata kutoka kwenye mazingira na shughuli wanazofanya.
Hapa nitaelezea tabia 10 ambazo ni dalili tosha kwamba wewe ni mjasiriamali. Kama huna tabia hizi unaweza ukaanza kujifunza taratibu na baadae ukawa na tabia za kijasiriamali. Kumbuka tofauti kubwa ya mjasiriamali ni jinsi anavyofikiri na kuchukua hatua tofauti na watu wengine. Kwa mfano wakati mwajiriwa anaweza kukubaliana na shida anazopata kwenye ajira yake na kuona hakuna anachoweza kufanya, mjasiriamali anafikiria uwezo wa tofauti alionao na jinsi anavyoweza kwenda kuutumia nje ya ajira na akafanikiwa. Baada ya hapo anaweza kuacha kazi na kwenda kufanya lile litakalomridhisha. Kwa kuwa na mtizamo chanya na utayari wa kuchukua hatua kunawafanya wajasiriamali kupata mafanikio makubwa.
Kama unatabia hizi 10, ni dalili tosha kwamba wewe ni mjasiriamali, unatakiwa kuchukua hatua mara moja ili kufikia mafanikio makubwa;
1. Hukubaliani na mfumo. Mara nyingi umekuwa ukihoji kwa nini kitu fulani kifanyike na umekuwa ukijitahidi kutafuta njia bora zaidi ya kufanya kazi fulani pale unapokuwa umeajiriwa. Hufanyi kitu bila ya kuhoji umuhimu wake na kufikiri njia ya kuboresha.
2. Unaonekana kama mfanyakazi mkorofi. Wakati mwingine umeshafukuzwa kazi mara kadhaa kutokana na tabia yako ya kuhoji na kutaka kuboresha utendaji kazi. Au umeshaacha kazi au kupanga kufanya hivyo kutokana na kutoridhishwa na kazi hiyo.
3. Una hamasa kubwa ya kutekeleza majukumu yako. Husubiri upangiwe cha kufanya, unajua majukumu yako na unayafanya kwa ubora wa hali ya juu.
4. Ukiambiwa hapana huridhiki, hapana sio jibu kwako unaendelea kutafuta njia nyingine mpaka upate NDIYO.
5. Unajiamini na unaamini una uwezo mkubwa wa kufanya mambo makubwa. Una uhakika hata kitokee kitu gani bado unauwezo wa kusimama na kuleta tofauti.
6. Ni mtu wa watu, unaweza kuchangamana na watu wa aina zote. Huna ubaguzi wa aina gani ya watu unaweza kukaa nao, popote unapokutana na watu unaweza kuanzisha mazungumzo na mkaenda vizuri.
7. Huogopi sana juu ya usalama wa ajira kwani unaamini hata bila ya ajira bado unaweza kuendesha maisha yako.
8. Mara kadhaa umekuwa ukigomea mamlaka. Umekuwa ukikataa maelekezo yanayotolewa na mamlaka kama hayaendani na misimamo yako ya ufanyaji kazi bora. Hii imekupelekea kuonekana ni mfanyakazi mkorofi na hata kufukuzwa.
9. Siku za mapumziko kama sikukuu au mwisho wa wiki ndio siku bora kwako kufanya kazi zako binafsi, huendekezi kupoteza muda kwa kupumzika au kustarehe.
10. Umewahi kuuza vitu vidogo vidogo ulipokuwa mtoto. Pia umewahi kufuga kuku, sungura na hata njiwa enzi za utotini.