Katika hali ya kawaida yale mambo madogo madogo ambayo watu wengi huyadharau ndio mambo ambayo yanawasababishia athari kubwa sana katika maisha ya kila siku. Ndio maana mbu ni mdogo lakini anasumbua sana katika maisha ya binadamu na kusababisha vifo vingi kwa watu licha ya udogo aliokuwa nao ambao analeta ugonjwa wa malaria.
VITU VIDOGO VIDOGO NDIO VINATENGENEZA AU KUBOMOA MAISHA YAKO.
Kuna usemi mmoja kutoka kwa mwandishi na mtunzi wa kitabu cha The Compound Effect ambaye anaitwa Darren Hardy anasema hivi ‘’ tembo hang’ati lakini mbu anang’ata’. Hivyo basi tunajifunza kuwa yale mambo madogo madogo au makosa madogo madogo ambayo watu wanayadharau ndio yanawaletea athari kubwa sana katika maisha yao ya kila siku.
Kuishi kuthibitisha katika yale unayoyafanya ndio njia kuu ya mafanikio lakini kuishi bila ya kuthibitisha katika yale unayoyafanya siyo njia kuu ya mafanikio. Kwa hiyo huna budi kuyatatua yale matatizo madogo ambayo unayadharau kila siku bila kujua ndio yanakuzuia kufikia katika mafanikio yako ya kila siku. Matatizo madogo haya unayoyadharau ndiyo yanakuvuta nyuma usiende mbele ni wakati sasa wa kutathimini ni kitu gani ambacho kinakuvuta nyuma kila siku na kutofikia katika mafanikio makubwa.
Kuna mambo mengi sana madogo madogo ambayo yanawazuia watu wengi kutofikia mafanikio na baadhi ya hayo ni kama yafutavyo;
1. Uvivu
Uvivu umekuwa ni changamoto sana kwa watu wengi na uvivu una leta athari sana katika maendeleo binafsi na ujenzi wa taifa kiujumla. Maisha ya mtu hayawezi kuendelea kama mtu ni mvivu na serikali inamtegemea mwananchi ili iweze kuendelea kama watu ni wavivu wa kufanya kazi, wavivu hata wa kufikiri kuendelea kuwa na fikra hasi ambazo hazileti matokeo chanya ni uvivu pia. Hivyo basi uvivu ni kitu kidogo sana lakini kila leta matokeo hasi kwa maisha ya binadamu.
2. Kufanya kitu Kimazoea
Kuendelea kufanya kitu kimazoea bila kuchukua hatua ya mabadiliko yoyote na kuona kuwa ni jambo dogo sana kumbe ndio linakuletea athari mfano unafanya biashara kimazoea badala ya kufanya mabadiliko. Mabadiliko yapo kila siku na yataendelea kuwepo kwa hiyo kuendelea kufanya kitu kile kila siku ndio kupoteza fursa mwandishi wa kitabu cha Jinsi ya Kufaidika na Mabadiliko Yanayotokea kwenye Maisha Makirita Amani ‘’anasema mabadiliko yalikuwepo, yapo nayataendelea kuwepo’’ hivyo basi usidharau mabadiliko madogo madogo ndiyo yanakupa athari katika Nyanja zote za maisha.
3. Kutojali Muda
Katika rasilimali ambayo tumepewa bure ni muda. Kila mtu ni tajiri wa muda hapa duniani kwa utajiri wa muda wote tuna masaa 24 lakini utofauti unakuja pale unavyoutumia muda wako vibaya ndivyo unakuwa masikini wa kutotumia muda vizuri. Makala nyingi na vitabu vingi wanasisitiza kuhusu muda, muda ndio rasilimali ambayo ikipotea hairudi tena. Kuendelea kutumia muda vibaya na kudharau ndio jambo linalokurudisha nyuma na siyo kitu kingine litatue sasa acha kulidharau.
4. Kutopenda Kujifunza
Ukitaka kufanikiwa kwanza anza kuwekeza katika maarifa. Huwezi kuendelea kama huna maarifa, watu hawapendi kujifunza kama kusoma vitabu, makala mbalimbali, kuhudhuria semina nakadhalika maarifa yamefichwa katika vitabu na kuendelea kukaa bila kuchukua hatua unapitwa na mengi, Kwa hiyo kuendelea kukaa bila kujifunza ndio moja wapo ya mambo madogo yanayokupa athari katika maisha.
5. Kuanza Siku bila kuwa na Ratiba
Kuanza siku bila kuwa na ratiba ni kukosa mwongozo wa siku nzima. Ratiba ni muhimu sana kwa binadamu ili kuweza kutimiza malengo yako ya siku bila mwingiliano wowote. Kuna watu wanadharau kuona kuwa ratiba ni jambo dogo lakini bila kujua kuwa lina muathiri sana katika maisha ya kila siku. anza siku yako na ratiba ni njia nzuri ya kutumia muda wako vema.
6. Kuishi bila Malengo
Mtu yoyote anayeishi bila malengo hapa duniani ni sawa na mtu anayekwenda safari hajui anapokwenda. Maisha ni malengo kama huna malengo huna maisha na dira ya maisha yako ni malengo ambayo yatakusaidia kukufikisha katika safari ya mafanikio.
7. Kuahirisha Mambo
Kwanza kabisa binadamu ametawaliwa sana na kuahirisha mambo. Kuahirisha mambo ni mwizi wa muda wetu, kila siku ni kuahirisha mambo tu ambayo yangeweza kubadili maisha yako kiujumla je unafikiri tabia hii itakuletea matokeo chanya katika maisha?
Kwa hiyo mambo madogo madogo ni mengi sana ambayo yanaleta athari kubwa ni vema kuyakabili mapema. kutokuwa mwaminifu katika maisha yako, umbea na majungu, kutoweka akiba, kukaa chini zaidi ya masaa 6 ni hatari bila kujishughulisha, kukosa kulala usingizi mzuri, kutokuwa na nidhamu na mengine mengi.
No comments:
Post a Comment