Thursday, 29 December 2016

Mbinu 10 za kufaulu Mitihani.

Mwanafunzi ambaye anataka kupata alama za juu katika mtihani wake lazima awe mtu wa kujiandaa kila siku kwa kutumia dondoo zifuatazo ili kujihakikishia uwezo wa kufaulu na kuepukana na dhana ya kuishi kwa kutegemea bahati.

 KWANZA: Kama nilivyosema hapo juu jambo la kwanza ni kuzingatia muda, si vema kukurupuka na kukimbizana nao na kujinyima usingizi wakati ratiba ya mtihani ilikuwa inafahamika na muhusika alikuwa na uwezo wa kujiandaa taratibu kuelekea kwenye siku ya kutahiniwa kwake.

 PILI: Jindae mwenyewe kwa kutafuta na kufanya mitihani iliyopita, huku ukinakili maswali ambayo watunzi wamekuwa wakiyarudia rudia kila mwaka.

 Njia hii itakuwezesha kujiandaa kwa kuzingatia shabaha na mahitaji halisi ya maswali yatokayo mara nyingi kwenye mitihani.  Hakikisha unapata mitihani ya nyuma ya ngazi uliyopo isiyopungua kumi au zaidi na uifanye huku ukihakikisha hakuna swali hata moja ambalo linakushinda.

 Pamoja na ukweli kwamba ubahatishaji wa vitu si njia sahihi sana, lakini umeonekana kuwasaidia wale ambao ubahatishaji wao huambatana na umakini, hivyo mwanafunzi anatakiwa kuwa na tabia ya kubahatisha maswali ambayo anadhani mwalimu wake anaweza kuyatoa kutoka kwenye daftari lake na hivyo kujiandaa.

 Ubaharishaji huu, lazima uambane na kile nilichosema awali, yaani  kuwa na kumbukumbu ya mitihani iliyopita. Wanasema watalaamu kuwa ulimwengu una tabia ya kurudia matukio, hivyo hata kwenye maswali kuna tabia hii ya kujirudia rudia.

 TATU: Orodhesha maeneo yote ambayo huyaelewi kwenye mtihani hiyo ya nyuma na uyafanyie mazoezi kwa kupata ushauri kwa waalimu wako. Kama kuna mada ambazo hujazielewa kwenye daftari lako hakikisha muda uliojiwekea utatosha kuzielewa.

 NNE: Hakikisha unajizoeza kufanya mitihani ya majaribio  mara kwa mara, ambayo utaifanya kwa kuzingatia muda na masharti yote ambayo hutolewa siku ya kufanya mtihani halisi.

Haifai mwanafunzi kukimbia majaribio yanayotolewa darasani na mwalimu wake, kwani hayo ndiyo yatamuwezesha kufahamu kama amekamilika kwa kutahiniwa au bado kuna eneo linamtatiza.

  TANO: Hakikisha kuwa kumbukumbu zako kichwani zinaongezeka kadiri unavyojifunza, usiwe mtu wa kusahau sahau uliyojifunza na ikiwezekana eneo ambalo unaonekana kulisahau ndilo ulipe kipaumbele cha kujikumbusha, ikibidi hata kila siku.

 SITA: Angalia kwa makini alama zako za mitihani ya majaribio, ikiwa unapata alama za chini ujue kuna mahali panahitaji nguvu za ziada, shauriana na mwalimu wako maeneo yote unayokosa au yanayokusumbua kabla ya siku ya mtihani.

 SABA: Ili mwanafunzi awe na uhakika wa kufanya vema mtihani wake anatakiwa kuzingatia dondoo zote zilizotolewa kwenye kipengele cha kuimarisha kumbukumbu kichwani, ambazo zimo ndani ya kitabu hiki.

   NANE: Wakati mwingine ni vema ukausikiliza mwili, si vema kuulazimisha kusoma hata kama unaona kuna udhaifu:
baadhi ya wanafunzi hukesha wiki mbili mfululizo wakisoma, matokeo yake mwili na akili huchoka na kushindwa kupokea masomo vizuri. Muda wa kupumzika unahitajika.

 TISA: Kabla mwanafunzi hajaingia katika chumba cha mtihani anatakiwa kujiamini kwa kushinda hofu:
Eneo hili ni muhimu sana kwani kuna wanafunzi hufeli si kwa sababu hawakujiandaa, bali hukumbwa na hofu muda mfupi kabla ya kuanza mtihani.
Hivyo ni muhimu mwanafunzi akaandaliwa kisaikolojia na waalimu pamoja na wazazi wake jinsi atakavyoweza kufanya mtihani bila hofu.

 KUMI: Imani ni hitimisho la mafanikio ya mwanafunzi:
haifai kuingia katika chumba cha mtihani ukiwa na mawazo hasi.

Kinachotakiwa ni ari ya ushindi au kwa lugha nyingine ni mawazo chanya. “LAZIMA NIFAULU MTIHANI HUU” Imani hii inaweza kujengwa na mtu kupitia kujiamini mwenyewe au kuamini kwa msaada wa nguvu za imani yake ya dini.

Kama unatabia hizi 10 basi tayari wewe ni Mjasiriamali.

Kwa muda mrefu kumekuwa na mjadala mkubwa ikiwa mjasiriamali anazaliwa au anatengenezwa. Kwa kuangalia tabia za wajasiriamali na tabia za binadamu kwa ujumla, wajasiriamali wana tabia za kipekee. Wajasiriamali wanafikiri tofauti na wanatenda tofauti na watu wengine kwenye jamii.

Tabia za kipekee zinazooneshwa na wajasiriamali kuna ambao wamezaliwa nazo na kuna ambao wamezipata kutoka kwenye mazingira na shughuli wanazofanya.

Hapa nitaelezea tabia 10 ambazo ni dalili tosha kwamba wewe ni mjasiriamali. Kama huna tabia hizi unaweza ukaanza kujifunza taratibu na baadae ukawa na tabia za kijasiriamali. Kumbuka tofauti kubwa ya mjasiriamali ni jinsi anavyofikiri na kuchukua hatua tofauti na watu wengine. Kwa mfano wakati mwajiriwa anaweza kukubaliana na shida anazopata kwenye ajira yake na kuona hakuna anachoweza kufanya, mjasiriamali anafikiria uwezo wa tofauti alionao na jinsi anavyoweza kwenda kuutumia nje ya ajira na akafanikiwa. Baada ya hapo anaweza kuacha kazi na kwenda kufanya lile litakalomridhisha. Kwa kuwa na mtizamo chanya na utayari wa kuchukua hatua kunawafanya wajasiriamali kupata mafanikio makubwa.

Kama unatabia hizi 10, ni dalili tosha kwamba wewe ni mjasiriamali, unatakiwa kuchukua hatua mara moja ili kufikia mafanikio makubwa;

1. Hukubaliani na mfumo. Mara nyingi umekuwa ukihoji kwa nini kitu fulani kifanyike na umekuwa ukijitahidi kutafuta njia bora zaidi ya kufanya kazi fulani pale unapokuwa umeajiriwa. Hufanyi kitu bila ya kuhoji umuhimu wake na kufikiri njia ya kuboresha.

2. Unaonekana kama mfanyakazi mkorofi. Wakati mwingine umeshafukuzwa kazi mara kadhaa kutokana na tabia yako ya kuhoji na kutaka kuboresha utendaji kazi. Au umeshaacha kazi au kupanga kufanya hivyo kutokana na kutoridhishwa na kazi hiyo.

3. Una hamasa kubwa ya kutekeleza majukumu yako. Husubiri upangiwe cha kufanya, unajua majukumu yako na unayafanya kwa ubora wa hali ya juu.

4. Ukiambiwa hapana huridhiki, hapana sio jibu kwako unaendelea kutafuta njia nyingine mpaka upate NDIYO.

5. Unajiamini na unaamini una uwezo mkubwa wa kufanya mambo makubwa. Una uhakika hata kitokee kitu gani bado unauwezo wa kusimama na kuleta tofauti.

6. Ni mtu wa watu, unaweza kuchangamana na watu wa aina zote. Huna ubaguzi wa aina gani ya watu unaweza kukaa nao, popote unapokutana na watu unaweza kuanzisha mazungumzo na mkaenda vizuri.

7. Huogopi sana juu ya usalama wa ajira kwani unaamini hata bila ya ajira bado unaweza kuendesha maisha yako.

8. Mara kadhaa umekuwa ukigomea mamlaka. Umekuwa ukikataa maelekezo yanayotolewa na mamlaka kama hayaendani na misimamo yako ya ufanyaji kazi bora. Hii imekupelekea kuonekana ni mfanyakazi mkorofi na hata kufukuzwa.

9. Siku za mapumziko kama sikukuu au mwisho wa wiki ndio siku bora kwako kufanya kazi zako binafsi, huendekezi kupoteza muda kwa kupumzika au kustarehe.

10. Umewahi kuuza vitu vidogo vidogo ulipokuwa mtoto. Pia umewahi kufuga kuku, sungura na hata njiwa enzi za utotini.


Ni mambo madogo sana ila yatakukwamisha kufikia malengo makubwa zaidi.


Katika hali ya kawaida yale mambo madogo madogo ambayo watu wengi huyadharau ndio mambo ambayo yanawasababishia athari kubwa sana katika maisha ya kila siku. Ndio maana mbu ni mdogo lakini anasumbua sana katika maisha ya binadamu na kusababisha vifo vingi kwa watu licha ya udogo aliokuwa nao ambao analeta ugonjwa wa malaria. 
VITU VIDOGO VIDOGO NDIO VINATENGENEZA AU KUBOMOA MAISHA YAKO.
Kuna usemi mmoja kutoka kwa mwandishi na mtunzi wa kitabu cha The Compound Effect ambaye anaitwa Darren Hardy anasema hivi ‘’ tembo hang’ati lakini mbu anang’ata’. Hivyo basi tunajifunza kuwa yale mambo madogo madogo au makosa madogo madogo ambayo watu wanayadharau ndio yanawaletea athari kubwa sana katika maisha yao ya kila siku.

Kuishi kuthibitisha katika yale unayoyafanya ndio njia kuu ya mafanikio lakini kuishi bila ya kuthibitisha katika yale unayoyafanya siyo njia kuu ya mafanikio. Kwa hiyo huna budi kuyatatua yale matatizo madogo ambayo unayadharau kila siku bila kujua ndio yanakuzuia kufikia katika mafanikio yako ya kila siku. Matatizo madogo haya unayoyadharau ndiyo yanakuvuta nyuma usiende mbele ni wakati sasa wa kutathimini ni kitu gani ambacho kinakuvuta nyuma kila siku na kutofikia katika mafanikio makubwa. 
Kuna mambo mengi sana madogo madogo ambayo yanawazuia watu wengi kutofikia mafanikio na baadhi ya hayo ni kama yafutavyo; 

1. Uvivu 
Uvivu umekuwa ni changamoto sana kwa watu wengi na uvivu una leta athari sana katika maendeleo binafsi na ujenzi wa taifa kiujumla. Maisha ya mtu hayawezi kuendelea kama mtu ni mvivu na serikali inamtegemea mwananchi ili iweze kuendelea kama watu ni wavivu wa kufanya kazi, wavivu hata wa kufikiri kuendelea kuwa na fikra hasi ambazo hazileti matokeo chanya ni uvivu pia. Hivyo basi uvivu ni kitu kidogo sana lakini kila leta matokeo hasi kwa maisha ya binadamu. 

2. Kufanya kitu Kimazoea 
Kuendelea kufanya kitu kimazoea bila kuchukua hatua ya mabadiliko yoyote na kuona kuwa ni jambo dogo sana kumbe ndio linakuletea athari mfano unafanya biashara kimazoea badala ya kufanya mabadiliko. Mabadiliko yapo kila siku na yataendelea kuwepo kwa hiyo kuendelea kufanya kitu kile kila siku ndio kupoteza fursa mwandishi wa kitabu cha Jinsi ya Kufaidika na Mabadiliko Yanayotokea kwenye Maisha Makirita Amani ‘’anasema mabadiliko yalikuwepo, yapo nayataendelea kuwepo’’ hivyo basi usidharau mabadiliko madogo madogo ndiyo yanakupa athari katika Nyanja zote za maisha. 

3. Kutojali Muda 
Katika rasilimali ambayo tumepewa bure ni muda. Kila mtu ni tajiri wa muda hapa duniani kwa utajiri wa muda wote tuna masaa 24 lakini utofauti unakuja pale unavyoutumia muda wako vibaya ndivyo unakuwa masikini wa kutotumia muda vizuri. Makala nyingi na vitabu vingi wanasisitiza kuhusu muda, muda ndio rasilimali ambayo ikipotea hairudi tena. Kuendelea kutumia muda vibaya na kudharau ndio jambo linalokurudisha nyuma na siyo kitu kingine litatue sasa acha kulidharau. 

4. Kutopenda Kujifunza 
Ukitaka kufanikiwa kwanza anza kuwekeza katika maarifa. Huwezi kuendelea kama huna maarifa, watu hawapendi kujifunza kama kusoma vitabu, makala mbalimbali, kuhudhuria semina nakadhalika maarifa yamefichwa katika vitabu na kuendelea kukaa bila kuchukua hatua unapitwa na mengi, Kwa hiyo kuendelea kukaa bila kujifunza ndio moja wapo ya mambo madogo yanayokupa athari katika maisha.

5. Kuanza Siku bila kuwa na Ratiba 
Kuanza siku bila kuwa na ratiba ni kukosa mwongozo wa siku nzima. Ratiba ni muhimu sana kwa binadamu ili kuweza kutimiza malengo yako ya siku bila mwingiliano wowote. Kuna watu wanadharau kuona kuwa ratiba ni jambo dogo lakini bila kujua kuwa lina muathiri sana katika maisha ya kila siku. anza siku yako na ratiba ni njia nzuri ya kutumia muda wako vema. 

6. Kuishi bila Malengo 
Mtu yoyote anayeishi bila malengo hapa duniani ni sawa na mtu anayekwenda safari hajui anapokwenda. Maisha ni malengo kama huna malengo huna maisha na dira ya maisha yako ni malengo ambayo yatakusaidia kukufikisha katika safari ya mafanikio. 

7. Kuahirisha Mambo 
Kwanza kabisa binadamu ametawaliwa sana na kuahirisha mambo. Kuahirisha mambo ni mwizi wa muda wetu, kila siku ni kuahirisha mambo tu ambayo yangeweza kubadili maisha yako kiujumla je unafikiri tabia hii itakuletea matokeo chanya katika maisha? 
Kwa hiyo mambo madogo madogo ni mengi sana ambayo yanaleta athari kubwa ni vema kuyakabili mapema. kutokuwa mwaminifu katika maisha yako, umbea na majungu, kutoweka akiba, kukaa chini zaidi ya masaa 6 ni hatari bila kujishughulisha, kukosa kulala usingizi mzuri, kutokuwa na nidhamu na mengine mengi. 

Misingi 6 iliyosiri ya watu wenye mafanikio ya kudumu.

Ili uweze kufanikiwa, ni lazima kujiwekea misingi imara ya kimafanikio itakayokuwa ikukuongoza kila siku. Bila kuijua misingi hii mapema sitashangaa kuona maisha yako yakibaki kuwa yaleyale bila ya kubadilika sana. Kwa kujiwekea misingi hii, inauwezo wa kufanya maisha yako kubadilika kwa sehemu kubwa sana.

Kama misingi hiyo ipo, ni nini kinachokuzuia wewe kufanikiwa sasa? Bila shaka hakuna. Unachohitajika kukifanya ni kutumia misingi hiyo mpaka kufanikiwa. Uwezo na nguvu za kubadilisha maisha yako kwa kadri unavyotaka unao. Kwa kuijua misingi hii, kwako itakuwa chachu ya kukusaidia kuweza kusonga mbele na kujijengea maisha ya mafanikio makubwa:-

Je, misingi hiyo ni ipi?

Hii Ndiyo Misingi 6 Muhimu Ya Kujiwekea, Ili Kujenga Mafanikio Ya Kudumu

1. Kaa mbali na watu hasi

Kama vile ambavyo ilivyo kompyuta inaweza ikaharibiwa na virusi na kuharibika kabisa, hata wewe maisha yako yanaweza kuharibiwa vivyohivyo lakini ikiwa una watu hawa hasi wengi wanaokuzunguka. Unapokuwa na watu hasi inakuwa ni rahisi sana kwako kuweza kuua mipango na malengo mazuri uliyojiwekea.

Ninajua watu hawa wanaweza wakawa ni rafiki zako au ndugu kabisa, lakini hiyo haina namna tena kwako, zaidi ya kuachana nao. Ikiwa utaendelea kung’ang’ania kuwa na watu hawa hasi utarudishwa nyuma sana katika maisha yako. Ili kuokoa maisha yako ni lazima kukaa mbali nao na kutafuta marafiki chanya watakaokupa hamasa ya kufanikiwa zaidi. Kukaa mbali na watu hasi ni msingi mzuri kwako unaotakiwa kuujua.

2. Wekeza kila siku katika maisha yako

Huu ni msingi muhimu sana kujiwekea ili kuwa na mafanikio ya viwango vya juu. Kama katika maisha yako unawekeza kila siku, tambua baada ya muda kidogo kuanzia sasa utakuwa mbali sana kimafanikio. Pengine unaweza ukaanza kusema ‘oooh mimi sasa sina pesa, sina mtaji hili halinihusu nitawekeza vipi sasa hapa?’

Sikiliza, hauhitaji kuwa na pesa ili kuwekeza. Anza na kuwekeza kwanza kwenye akili yako kwa kujifunza kupitia vitabu au semina mbalimbali. Maisha yako yatakuwa ya thamani sana kila utakavyozidi kufanya uwekezaji huu. Maarifa utakayoyapata huko kwani yataweza kukusaidia kuwekeza katika maeneo mengine na kufanikiwa zaidi pale utakapopata mtaji unaouhitaji.

3. Kuwa wewe kama wewe

Kuna wakati wengi wetu huwa ni watu wa kutaka maisha ya kuwapendezesha wengine. Nikiwa na maana kutaka kuishi maisha kama wengine wanavyoishi. Hiki ni kitu hatari sana kwako kwa sababu unakuwa unaishi kwa kufuata bendera ama wengine wanavyoishi na kujikuta unakuwa mtu wa kupoteza mwelekeo.

Ili uweze kuishi kwa mafanikio ni vizuri ukajijengea msingi wa kuishi maisha yako ukiwa wewe kama wewe. Kwa kuishi wewe kama wewe itakulazimisha kutambua unataka nini kwenye haya maisha, ni lini utafikia mipango yako uliyojiwekea na unataka kitu gani kikusaidie kufikia malengo yako. Huo ndiyo msingi muhimu pia kuujua kwa ajili ya mafanikio yako ya leo na kesho.

4. Jiwekee mipaka katika maisha yako

Ishi maisha yako kwa kujiwekea mipaka. Usije ukaruhusu kila mtu kuingilia maisha yako kwa jinsi anavyotaka hata awe ndugu wa karibu kiasi gani. Bila shaka umeshawahi kuona watu ambao maisha yao yanaharibiwa kutokana na kuingiliwa na watu walio karibu nao. Na hii yote imekuwa ikitokea kutokana na wahusika kushindwa kujiwekea mipaka iliyoimara katika maisha yao.

Mipaka hii unatakiwa ujiwekee katika maeneo mabalimbali kama vile katika muda, kazi zako za kawaida na wakati mwingine kwenye biashara zako unazozifanya. Kwa kufanya hivyo watu wako wa karibu watakuwa hawako huru sana kuingilia yale maeneo uliyojiwekea mipaka maana wakifanya hivyo watajua utakuwa mkali au hutakubali kiurahisi. Hiyo itakusaidia kukujengea msingi mwingine imara wa mafanikio yako.

5. Kuwa king’ang’anizi wa mafanikio

Kwenye maisha yako kitu ambacho hutakiwi kukiruhusu ni kushindwa kiurahisi. Kama ikitokea umeshindwa katika jambo kwa namna moja au nyingne, jaribu kutafuta njia ya kulifanya jambo hilo kwa namna ya tofauti mpaka kufanikiwa. Unapokuwa king’anga’nizi wa mafanikio huo utakuwa msingi bora kwako unaojitengenezea wa kufikia mafaniko makubwa.

Maisha ni kusonga mbele. Ng’ang’ania mafanikio yako mpaka uyaone hata kwa gharama yoyote ile. Usiruhusu kitu kikakukatisha tamaa. Kama unafikira za nyuma unazoziweza kwa kudhani kuwa ulikosea eneo fulani ni bora ukaachana nazo fikra hizo kwa sasa, kwa sababu hazitakusaidi kitu chochote zaidi ya kukwamisha wewe. Yaliyopita yamepita, songa mbele.

6. Jijengee ukomavu wa fikra

Ili uweze kufanikiwa inatakiwa ifike mahali fikra zako ziwe zimekomaa na kuweza kutambua kila hali inayojitokeza katika maisha na jinsi ya kuweza kukabiliana nayo. Kwa mfano, inapotokea kushindwa au ukakosea katika jambo fulani, unakabiliana vipi na kushindwa huko bila kuumia au kujiona hufai na kisha kuendelea mbele?

Hakuna kingine zaidi ya wewe kuwa na ukomavu fulani wa fikra utakaokuwezesha kusonga mbele. Ukomavu huu ni rahisi kuupata, utaupata tu ikiwa wewe ni mtu wa kujifunza mambo mbalimbali ya kimafanikio kama unavyofanya sasa hivi. Bila kufanya hivyo hutaweza kuhimili mawimbi mengi ya maisha yanayojitokeza kwa upande wako.

Kumbuka hii ni sehemu ya misingi ambayo unaweza ukajiwekea kama nguzo ya mafanikio yako. Lakini, kwa kutumia kijitabu chako kidogo cha kujifunzia unaweza ukaongeza misingi mingine ambayo unaona kwako inafaa kukuongoza katika safari ya mafanikio. Bila kujiwekea misingi binafsi, utayumbishwa sana katika maisha kwa mambo mengi na itakuwa ngumu kufanikiwa.

Man U transfer Rumours..

United have been handed a boost in their pursuit of James Rodriguez, with The Daily Star suggesting Real Madrid will lower their £50 million asking price in the summer - but not this January.

Antoine Griezmann is reportedly United's No 1 target, but Atletico Madrid are reluctant to sell and should it prove impossible to lure the Frenchman away from the Vicente Calderón, James is next on the list.

James has repeatedly discussed his future in public - much to Real's annoyance - and they have supposedly asked the Colombian forward to stay in line for the rest of the season.

James Rodriguez is being linked with UnitedCREDIT: REX FEATURES

He is quoted in The Star as saying: "I can't guarantee that I'll stay at Real Madrid after the winter window."

Man Utd have no intention of allowing Anthony Martial to leave Old Trafford on loan next month, reveals today's Telegraph.

Martial has struggled to hold down a starting place during a difficult second season at United and Philippe Lamboley, the France forward's agent, has claimed they have been exploring the possibility of the player joining Sevilla on loan until the end of the season.

Lamboley told ABCdeSevilla: "We are studying the Sevilla option in detail. Sevilla are a very good club, are in a good position in La Liga, play in the Champions League and have a great coach. That's all I can tell."

Anthony Martial is wanted by Sevilla CREDIT: AP

United, however, are adamant that Martial forms an important part of manager Jose Mourinho's plans and will give no consideration to letting him leave on loan in the transfer window next month.

Valencia have made a bid to sign Man Utd defender Marcos Rojo, according to Calciomercato. We are told the offer for the Argentina international is in the region of €16 million (about £13.5 million).

It had looked like Rojo's future at Old Trafford was over after a number of unconvincing performances since his arrival, but a recent upturn in form and fitness has seen his stock rise to the point where The Daily Mail is reporting that Manchester United have cooled their interest in Benfica's £38 million-rated defender Victor Lindelof.

The Mail suggests Jose Mourinho has been impressed by the partnership of Phil Jones and Rojo in the absence of Chris Smalling and Eric Bailly, who are both also now available again after injury, and does not now see signing a new centre-back in the January transfer window as a priority.

Jose Mourinho has cooled his interest in Victor Lindelof CREDIT: REX FEATURES

The Mail continues that Mourinho will only add to his squad next month if players go out, and Everton are expected to step up their pursuit of Morgan Schneiderlin andMemphis Depay next week. West Ham have lodged enquiries about the availability of Marouane Fellaini and Marcus Rashford.

United are one of the several clubs interested in Bayern Leverkusen star Julian Brandt, according to The Mail. 

The German international primarily appears on the left-wing, but he can also play as an attacking midfielder or on the right and would cost around £20 million.

And finally, former United star Juan Sebastian Veron is returning to football for a fifth spell with Argentine side Estudiantes... aged 41.

Veron is the club's president and has made good on a promise that he will play in the 2017 Copa Libertadores if fans buy 65 per cent of the tickets for the match. He will donate his minimal salary earned playing for Estudiantes back to the club.

Vinara wa kupiga pasi za mwisho EPL.

Ligi kuu ya England maarufu kama EPL huwa ina mabadiliko sana mchezaji anaweza akang’aa msimu mmoja msimu unaofuata akashindwa kutekeleza jukumu.

Hii ndivyo ilivyo mifano mizuri Jamie Vardy,  Ozil hata Hazard.

Msimu uliopita Ozil ndiye alikuwa kinara wa kutoa pasi za mwsho alipiga pasi 19 za magoli ambapo ilibaki moja afikishe rekodi ya Thiery Henry, japo haikuwa rahisi kwake kuzipata pasi zote hizo na huenda kama safu ya ushambuliaji ingetulia angeweza kuvuka rekodi ya Henry.

Hazard msimu uliopita hakuwa katika kiwango kizuri lakini msimu huu amerudi vyema sana, hivyo hivyo kwa Vardy alipata magoli 24 lakini msimu huu ametuama kama maji ya mtungi hii ndio maana halisi ya mchezo wa soka.

EPL YA 2016-2017

Hadi sasa Kevin De Bruyne ndiye kinara wa pasi za mwisho ana nafasi za usaidizi 9 na magoli 6 ya kufunga hivyo wastani mkubwa sana kwake ikiwa bado miezi mitano ligi iishe. Huku nafasi ya pili ibashikwa na Alexis Sanchez akiwa amepata kusaidia nafasi 6 akiwa sambamba na Adam Lalalana. Idadi hii kabla ya mechi za ‘Boxing Day’.

Ibrahimovic kufikia rekodi ya Messi desemba 31?

   Inawezekana mwaka huu ukawa mzuri kwa nyota wa Manchester United Zlatan Ibrahimaovic ama wanavyomuita Shivo katika vibanda umiza kutokana na kupiga karate mchezaji huyo na mazoezi ya ngumi sana huku akiwa na umri mkubwa lakini bado anasumbua mabeki wa timu pinzani.

Ametua Manchester United msimu huu na tayari amepachika magoli 12 ya ligi kuu ya EPL akiwa mshindi wa tatu akiwa sawa na Alexis Sanchez huku Diego Costa akiwa na magoli 13 mbele yao. Mchezaji huyu amekuwa akipiga magoli kwa mechi 3 mfululizo sasa huku akionekana mzuri wa katika 18.

Ibrahimovic amefikisha magoli 50 kwa mwaka huu yaani tangu uanze mwaka huu wa 2016 akizidiwa goli 1 na Lionel Messi huenda desemba 31 kama akifunga dhidi ya Middlesbrough basi atakuwa sawa na Messi.

Wakati huo huo Kocha wa Chelsea amewataka wachezaji wake kujitahidi ili kupata matokeo zaidi ili waweze kuchuku ubingwa, Klabu hiyo imeendeleza wimbi la ushindi wa ligi kuu ya England kwa mechi 12 mfululizo.

Chelsea iko nafasi ya kwanza ikiwa na alama 46 huku nafasi ya pili ambayo inashikiliwa na Manchester City ambayo ina alama 39 ikiwa nyuma kwa alama 7. Klabu hiyo inaenda sambamba na mfungaji wake Diego Costa akiwa na magoli 13 nyuma ya Sanchez na Ibrahimovic.

Dikteta wa North Korea afuta Sikukuu ya Mwaka Mpya.

Utakuwa umejipangaje kusherehekea siku kukuu ya mwaka mpya na ni wapi ? Ambapo bado siku 3 tuweze kuingia mwaka 2017,  Kama ulikuwa unataka kusherehekea sikukuu za mwaka mpya kwa namna yake basi utakuwa umekosea na huruhusiwi huko Korea Kaskazini.

Rais wa nchi hiyo Kim Jong Un amepiga marufuku sherehe za mwaka mpya amejaribu kufuta kuanzia siku ya Krismas ili kumuenzi Bibi aliyekuwa mwanaharakati wa nchi hiyo kipindi cha nyuma katika uongozi wa kikomonisti.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un amepiga marufuku sherehe za Krismasi na mwaka mpya kusherekewa nchini humo kwa mujibu wa habari ya India Times ni kuwa badala ya kusherekea kuzaliwa kwa Yesu kulingana na imani ya wakristo, raia nchini humo watatenga siku hiyo kumuenzi bibi ya Kim .

Kim ambaye pia ni mwanaharakati wa kikomunisti amefahamisha kuwa bibi yake atatambulika kuwa ‘Mama mtakatifu wa mabadiliko.

TRUMP: Umoja wa mataifa (UN) ni sawa na genge la wapiga Soga.

SIKU chache baada ya Umoja wa Mataifa (UN) kupiga kura kulaani ujenzi wa makazi ya walowezi wa Kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi na Yerusalem Mashariki, Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, amehoji ufanisi wa chombo hicho, akisema ni ‘genge la watu wakusanyikao na kupiga soga’.

Alitoa kauli hiyo baada ya jaribio lake la kutaka kupinga azimio lililokemea mpango wa Israel kuendelea kujenga makazi katika ardhi ya Wapalestina kushindikana.

Baraza la Usalama la UN (UNSC) limesema Israel inakiuka sheria za kimataifa kwa kujenga katika ardhi ya Wapelestina.

Azimio hilo lilipitishwa Ijumaa iliyopita, huku Trump akitoa onyo kuwa mambo yatakuwa tofauti wakati atakaposhika rasmi hatamu za uongozi wa Marekani.

Uamuzi wa utawala wa Rais Barack Obama kujiweka kando wakati UNSC ilipopiga kura hiyo ilihali ina kura ya turufu yenye uwezo wa kuitetea Israel, umekosolewa na Trump na kulaaniwa vikali na Israel.

Awali Desemba mwaka jana, Trump aliwahi kukaririwa akisema angependa kutoegemea upande wowote katika masuala ya Israel na Palestina.

Lakini msimamo wake ukawa ukibadilika kadiri kampeni za urais zilipoendelea akiegemea Israel zaidi.

Licha ya shutuma za Trump kwa UN, chombo hicho kwa miaka mingi kinashutumiwa na baadhi ya Serikali za magharibi kukosa ufanisi, huku mataifa yanayoendelea yakisema kinaburuzwa na mataifa tajiri.

Biashara tano unazoweza kufanya ukiwa na mtaji mdogo wa laki moja.

Mitaji imekuwa kikwazo kikubwa katika kuanza biashara nyingi sana. Sababu nyingine ni kuwa watu wengi wanaofikiria kuanza biashara wanataka kuanza na mitaji mikubwa kama milioni 5 -10 au zaidi. Ukweli ni kwamba hiyo ni ngumu hasa kwa nchi ambazo ni maskini kama Tanzania. Mwishowe mawazo mengi ya biashara yanakufa kabla ya kuanza. Wataalamu wa bishara wanaeleza kuwa kuanza ni kugumu na ni kikwazo kikubwa cha mafanikio ya wajasiliamali wengi Ukweli ni kuwa kuna biashara nyingi tu ambazo hazihitaji mitaji mikubwa kuanza.

1. Kufundisha:  Tafuta kitu ambacho unakifahamu na angalia jinsi utawapa watu elimu yako. Mfano unaweza ukawa ni mtaalamu wa kupika keki tamu. Basi unaweza ukaanda darasa la watu katika maeneo unayoishi na kuandaa mafunzo kwa ada ndogo nyumbani kwako. Unahitaji kiasi kidogo tu cha fedha ili kutimiza hilo. Pia unaweza ukafundisha watoto masomo ya ziada kama hesabu au sayansi kama unaufahamu wa masomo hayo au mengineyo. Vyote hivi havihitaji hela nyingi kuanza kwasababu huhitaji chumba cha biashara wala fanicha.

2. Biashara ya Mtandao Jiunge na kampuni inayofanya masoko kwa njia ya mtandao. Makampuni haya yatakuhitaji wewe kuafanya matangazo kwa njia ya mdomo kwa mtu hadi mtu kwa kuwaeleza juu ya bidhaa za kampuni husika na wakinunua basi kampuni itakulipa wewe kiasi cha fedha kwa mauzo yaliyofanyika. Usajili katika biashara hii kunahitaji mtaji mdogo sana hata kwa Sh. 100,000 tu unaweza ukaanza na kuendelea kukuza mtaji. Baadhi ya biashara za mtandao kuanza Trevo: Soma: Biashara ya Mtandao ya Trevo- Kwa Kuboresha Afya na Kipato Biashara ya Trevo – Biashara ya Mtaji Mdogo Chini ya TSh. 500,000 OneCoin: Soma : Fahamu Sarafu Mpya ya Kidigitali ya OneCoin na Fursa Zake,

3. Kutoa Ushauri wa Kitaalamu: Kama wewe ni mtaalamu katika nyanja fulani kama vile fedha,afya au komputa kwa mfano,unaweza ukaanzisha huduma ya ushauri kwa makampuni madogo au watu binafsi. Ili kufanya hivyo utahitaji fedha kidogo tu kwaajili ya vitendea kazi kama vile karatasi, kalamu n.k Utahitaji kujitangaza kwa kupita ofisi hadi ofisi au kwa kutoa matangzao katika radio ,TV au magazeti. Unaweza kutumia ofisi za wateja kwajili ya kazi hii hivyo kuwa na ofisi. Tumia sehemu unayoishi kama ofisi hivyo ngarama itakuwa ndogo sana.

4. Huduma ya Kutunza Watoto Wadogo : Kutunza watoto wadogo kati ya mwaka 1-5 ni biashara ambayo unaweza ukaianzisha na kuifanya nyumbani na itahitaji fedha kidogo tu. Wazazi wenye watoto wanahitaji sehemu ambayo watoto wao watapata huduma wao wakiwa kazini. Kama ukianda mazingira mazuri ampapo watoto wanaweza kucheza na kujifunza,basi utapata wateja wengi.

5. Kukodisha Hema : Huduma ya kukodisha hema kwaajili ya shughuli ni mijawapo ya biashara ambazo hazihitaji mitaji mikubwa. Utahitaji hema moja au mawili ili kuanza na kisha unaweza ukaongeza kadiri unavyoendelea na kukua. Uhitaji wa hudum hii ni mkubwa hasa katika shrehe za harusi,siku za kuzaliwa,kipaimara ,komunio,maulidi na bia katika shughuli za misiba.

Mwisho Biashara zote nilizozitaja hazihitaji fedha nyingi kuanza,kiukweli Shilingi 100,000 tu au pungufu zinatosha. Hivyo kama unafikiria kuanza bishara na huna mtaji wa kutosha;basi fikiria mojawapo kati ya hizi na ufanikiwe. Ningependa kusikia biashara nyingine kama hizi. Andika katika kisanduku cha maoni hapa chini nautume.

7 steps to having great Ideas.

So, the seven steps to having ideas are:

Step 1 – Gather your information

Information is the raw material from which ideas are born. There are two types of relevant information, specific and general.

General information includes just about anything and everything, and gathering it is a lifelong exercise. It basically comes down to general knowledge and education, and can be cultivated through the usual channels: reading widely and having an active interest in life and the world around you, and in particular in people, how they live, what they think and how they behave.

Specific information is directly relevant to the topic in hand. You clearly need to get all the specific information you can lay your hands on. If you’re writing an advert for a product or service, you would expect the client to come up with most of it, although you’ll probably want to do some of you own research as well. If you’re writing a blog post on a topic, you’ll need to gather your information from far and wide.

These days, gathering information is a much faster process thanks to the internet. The down side to that is you’ll need to be judicious, and discard that which isn’t really relevant. Otherwise, you’re likely to get overwhelmed during step 2, where you have to sift the information.

Step 2 – Sift the information

Work over the information, turning it over and around until you see how it all fits together. A direct pursuit of ‘meaning’ might be counterproductive. You may need to try a subtle approach, and sneak up on the topic, looking at things from various angles.

If small snippets of ideas start coming to you at this stage, write them down, even if they seem crazy.

The more you turn and sift the information, the better you understand it, the easier it will be to see and really understand the relationships. And the more ideas you will have.

Step 3 – Let the information bubble

The next stage is to let the information bubble away for a while, keep it on simmer in your mind. You need to let your unconscious mind work on it for a time. It’s a good idea to do something else for a while, to stimulate your imagination and emotions. Try reading, listening to music, meditate, go for a walk, while your mind digests the facts.

Or you could try the traditional approach – take a warm bath and wait for the eureka moment.

Step 4 – Eureka! Let the ideas flow

It’s at this stage that ideas should start to appear, as if from ‘nowhere’. This is where you hope for a ‘Eureka’ moment. The answer to your problem may appear to leap into your mind for no apparent reason.

But what if it doesn’t come? You keep going, writing down the best ideas you can come up with. If your ideas aren’t strong enough yet, don’t panic, because you’ll get to have another go at this part of the process. So take the very best ideas you can come up with, and move on to step five.

Step 5 – Shape and develop your idea

Now your idea needs to be shaped and moulded, turned into something real. This where your writing skills come to the fore.

Step 6 – Share your idea

Now show your idea to others and see what they think. They may be able to add to it and make it better. That may spark new ideas, and so the process becomes ever more creative.

Step 7 – Rinse and repeat

If necessary, use the feedback you got in step 6, and add that to the information you gathered in step 1. Now repeat step 2, sifting the new information with the existing facts. Then repeat steps 3, 4, 5 and 6.

Keep it going, until you have the best idea you can come up with, or you hit the deadline, and have to go with what you have developed so far.

So, the good news is that you can learn to be more creative and have stronger ideas. You:

Gather the informationSift itLet it percolateLet the ideas flowShape and mould the ideasShare them with othersPut the feedback into the loop; and repeat the process to strengthen your ideas.

That’s the good news. The bad news is, despite what I said at the start about the importance of ideas – and don’t get me wrong they are important – despite that, the truth is that having ideas is the easy part of writing.

Yes, ideas are easy. It’s the execution that is truly difficult, that’s where the real genius lies. And you can only master the craft of writing through hard work and long, steady perseverance.

Wednesday, 28 December 2016

Chuo cha marubani cha kimataifa kujengwa Mbeya.

Mbeya.Kiwanja kidogo cha ndege kilichopo katikati ya Jiji la Mbeya kinatarajiwa kujengwa chuo cha kimataifa cha marubani nchini.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (Taa), Laurent Mwigune ametoa taarifa hiyo kwenye mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, wananchi na viongozi wa Taa.

Awali, mkazi wa Kata ya Iyela, John Mwanguku alilalamikia eneo hilo kuwa ni la wazazi wao tangu mwaka 1977 na kwamba walikubaliana na wataalamu kuwapimia viwanja vya makazi vyenye hati miliki ili waviendeleze.

Mwanguku amesema walikubaliana na maofisa ardhi waifanye kazi ya kupima viwanja kwa maelewano ya kupewa viwanja 10 kati ya vitakavyopatikana ndani ya uwanja huo wa ndege.

Hata hivyo, Mwigune amesema uwanja wote wa ndege utaendelea kumilikiwa na Taa, pia wana mipango ya kujenga chuo cha kimataifa kufundishia marubani.

“Tumeshtushwa kupata taarifa za ugawaji wa viwanja kinyemela kwa kuwa uwanja huu bado uko mikononi mwetu, tunatarajia kujenga chuo cha kimataifa cha marubani ili kuiwezesha nchi kuwa na marubani wa kutosha,” amesema.

Kutokana na kauli hiyo, Makalla alilazimika kusitisha ugawaji wa viwanja hivyo baada ya kubaini kuwapo kwa vitendo vya rushwa.

Manchester United na Manchester City kukutana Marekani

Debi ya kwanza ya Manchester kuchezewa nje ya England huenda ikachezewa nchini Marekani majira yajayo ya joto.

City chini ya Pep Guardiola na United chini ya Jose Mourinho, walipangiwa kukutana mjini Beijing, Uchina Julai mwaka huu.

Hata hivyo, hilo halikufanyika baada ya mvua kubwa kunyesha na kuzuia mchezo huo kufanyika uwanja wa Bird's Nest. Debi ya Manchester yatibuka Mchezo huo ulifutiliwa mbali saa sita kabla ya kuanza. Klabu zote mbili zitakuwa Marekani Julai kujiandaa kwa mwanzo wa msimu wa 2017.

Hakujatolewa maelezo zaidi lakini klabu zote mbili zinatarajiwa kushiriki katika Kombe la Bingwa wa Kimataifa.

Orodha ya FIFA: Argentina yaongoza duniani, Senegal yawika Afrika

Taifa la Guinea-Bissau ndio taifa lililofaidika sana katika orodha mpya ya shirikisho la soka duniani Fifa mwaka 2016 baada ya kupanda nafasi 78 tangu Disemba mwaka uliopita.

Taifa hilo sasa limeorodheshwa la 68 katika orodha ya dunia na la 15 barani Afrika.

Hatua hiyo inamaanisha kwamba Guinea Bissau ipo juu ya mataifa ya Uganda ,Togo na Zimbabwe ambayo pia yamefuzu katika kombe la mataifa ya Afrika nchini Gabon.

Senegal inakamilisha mwaka huu ikiwa ndio taifa linaloongoza barani Afrika na nambari 33 duniani.

Guinea Bissau ilifuzu katika michuano ya mataifa ya Afrika baada ya kuishinda Kenya na Zambia mwaka 2016.

Walipoteza mechi yao ya mwisho dhidi ya Congo-Brazaville lakini ikafanikiwa kumaliza katika kilele cha jedwali ili kuweza kufuzu Gabon.

Katika orodha ya dunia Argentina bado inasalia katika nafasi ya kwanza.

Orodha ya mataifa ya Afrika duniani:

Senegal (33)

Ivory Coast (34)

Tunisia (35)

Egypt (36)

Algeria (38)

DR Congo(48)

Burkina Faso (50)

Nigeria (51) (hakufuzu Gabon 2017)

Ghana (53)

Morocco (57)

Roboti wa kushiriki ngono atatengenezwa mwakani.

Je ungependelea kushiriki ngono na roboti? ungefunga ndoa na roboti? na Je roboti anaweza kuwa na haki ya kupinga ndoa hiyo?

Haya ni baadhi ya maswala machache yanayoulizwa katika mkutano wa pili wa kuwa na mpenzi wa roboti mbali na kushiriki naye ngono katika chuo kikuu cha Goldsmith mjini London baada ya serikali ya Malaysia ambayo ndio iliokuwa taifa la maandalizi ya mkutano huo kuupiga marufuku.

Hatua hiyo imezua utata sio tu kwa mataifa yenye maoni ya Kihafidhina . Hakukuwepo na wawakilishi kutoka kwa sekta ya ngono wala roboti za ngono katika mkutano huo.

Ni watu wachache walioweza kusema kuwa roboti Pepe alikuwa na maumbile ya kuvutiai Kampuni ya Real Dolls inayotengeza wanaserere wa ngono ilidai kwamba itatengeza roboti wa ngono aliye na akili bandia mwaka ujao.

Uzinduzi huo iwapo utafanyika utakuwa ushahidi wa David Levy ambaye amekuwa akitabiri ujio wa roboti zinazofanana na binadamu zenye akili bandia.

Alitoa hotuba ya kufunga mkutano huo ambapo alipendekeza utengezaji wa roboti za ngono. ''Tuna roboti za urafiki na sasa roboti ambaye anaweza kuwa mpenzi ndio mtindo mpya''.

Kwa wengine kushiriki ngono na roboti ni ndoto yao lakini kwa wengine ni uharibifu mkubwa Katika kipindi cha miaka 10 ijayo, inawezakana kutengeza roboti ambayo watu wataihitaji kama mpenzi, ina upendo, inaaminika, inaheshima na hailalamiki alisema. Wengi watapendelea uhusiano huo wa roboti na huenda wakataka kufunga ndoa nao.

Mpango huo wa mpenzi wa aina ya roboti huenda akazua maswali kadhaa ya kimaadili, hususana wakati ambapo sheria italazimika kutambua roboti kama binaadamu.

Mourinho:Schneiderlin anaweza kuondoka.

Mkufunzi wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa yuko tayari kumruhusu kiungo wa kati wa Ufaransa Morgan Schneiderlin kuondoka katika klabu hiyo baada ya mchezaji huyo kutaka kufanya hivyo.

''Siwezi kumzuia mchezaji ambaye hana raha.Ingekuwa rahisi kumkataza iwapo ningekuwa namshirikisha kila mechi lakini kwa sababu anashiriki mara moja moja, basi sina budi kumwachilia kwenda iwapo ombi linaloletwa kwa Manchester United linavutia''.

Schneiderlin mwenye umri wa miaka 27 aliisaidia klabu ya Southampton katika mikutano kadhaa kati ya klabu hizo mbili hatua iliolazimu Manchester United kumsajili.

Ryan Giggs kuifunza Swansea?

Kiungo wa zamani wa Manchester United anatarajiwa kumrithi mkufunzi aaliyekuwa mkufunzi wa Swansea Bob Bradley, aliyetimuliwa usiku wa kuamkia leo na Klabu ya Swansea.

Awali, Giggs, mwenye umri wa miaka 43, alihojiwa mara mbili na timu hiyo kabla ya nafasi hiyo kuchukuliwa na Bradley mwezi Oktoba.

Bradley aliachishwa kazi baada ya kuiongoza Swansea kwa siku 85 pekee na kuiacha katika nafasi ya 19 kwenye ligi. Ingawa hana uzoefu mwingi, baada ya kustaafu, Giggs aliitumikia Manchester United chini ya David Moyes na kuwa naibu wa kocha, chini ya meneja wa zamani Louis van Gaal.

Nahodha huyo wa zamani wa Wales anadaiwa kufanya mazungumzo na wasimamizi wa Swansea, na mwenyekiti wa klabu hiyo, Huw Jenkins anadaiwa kuvutiwa na Giggs.

Naibu kocha wa Zamani wa United Rene Meulensteen, anaamini Giggs anatosha kuiongoza Swansea. "Siamini kuwa Giggs hana uzoefu, alipata ujuzi akiwa naibu mkufunzi chini ya Manchester United." Rene Aliiambia BBC Radio 5 Live.  

Wengine wanaosakwa na klabu hiyo ni meneja wa Wales, Chris Coleman, mkufunzi wa zamani wa Leicester City Nigel Pearson na aliyekuwa mkufunzi wa Birmingham City manager Gary Rowett.

Hata hivyo, Mrithi wa Bradley anatarajiwa kuchukua usukani baada ya mechi yao ya nyumbani dhidi ya Bournemouth mwisho wa mwezi. Kwa sasa, timu hiyo inayoongozwa na wakufunzi wa muda Alan Curtis na Paul Williams watainoa timu hiyo hadi uteuzi utakapofanywa.

Swansea ilipoteza mechi yake ya saba kati ya mechi 11 kwa kupata kichapo cha 4-1 dhidi ya West Ham ikiongozwa na Bradley Timu hiyo ina alama 12 baada ya kukusanya pointi 8 pekee na kufungwa mabao 29.

Guardiola:Ni vigumu Man City kuishika Chelsea.

City ilipanda hadi nafasi ya pili katika jedwali baada ya kuicharaza Hull City 3-0 katika siku kuu ya Boxing Dei na kuweza kuwa nyuma ya Chelsea kwa pointi 7. 

Kikosi hicho cha Antonio Conte awali kiliweka rekodi ya kushinda mara 12 katika ligi ya Uingereza baada ya kuichapa Bournemouth 3-0. ''Tumecheza mechi saba zaidi ya Chelsea ,ndio maana ni vigumu '',alisema Guradiola. 

''Liverpool ilikaribia taji hilo mwaka 
mmoja uliopita kwa sababu walikuwa na mechi moja kwa wiki ,na ni hivyo ndivyo ilivyokuwa na Leicester.Mara hii Chelsea na Liverpool wana fursa''. 

Liverpool na Chelsea zilishindwa kufuzu katika mashindano ya Ulaya baada ya kumaliza wa nane na 10 mtawalia katika ligi ya Uingereza mwaka uliopita.

Mwanamke aliyenusurika kifo baada ya kuanguka kutoka kwenye ndege aaga dunia

Kituo cha runinga cha taifa nyumbani kwa Vulovic nchini Serbia, kinasema kuwa, alipatikana akiwa amekufa nyumbani kwake mjini Belgrade.

Vulovic alikuwa akifanya kazi na shirika la ndege la Yugoslavia tarehe 26 mwezi Janauari mwaka 1972, wakati bomu lililipuka na kuangusha ndege kwenye milima ya Czechoslovakia.

Abiria wote 27 na wahudumu wa ndege waliangamia kwenye ajali hiyo. Kulingana na wachunguzi, Vulovic alikwama kwenye kigari cha chakula kwenye mkia wa ndege wakati ilianguka ardhini.

Ajali iliyomuua katibu mkuu wa UN kuchunguzwa Abiria 6 'walevi' wapigwa marufuku kuabiri ndege ya Jet2 Sehemu hiyo ya mkia wa ndege ilianguka eneo lenye miti mingi hali iliyookoa maisha yake.

Aliokolewa na mwanamume mmoja aliyekuwa eneo hilo baada ya kumsikia akilia gizani. Babda ya kuwasili hospitalini alipoteza fahamu kwa siku 10 na pia alikuwa na majeraha mabaya.

Ajali jiyo ilimwezesha mhudumu huyo kuandikwa kwenye kitabu cha kumbukumbu cha Guinness Book of Records mwaka 1985 kama mtu aliyeanguka umbali mkubwa zaidi na kunusurika bila kutumia mwavuli.

Netanyau aipinga hotuba ya Kerry kuhusu makazi.

Waziri Kerry amesema hatua hiyo ina nia ya kulinda uamuzi wa kuwepo kwa mataifa mawili ili kuzuia hatari ambayo ingeweza kutokea.          

Amesema bila ya usalama wa Israel na uwepo wa Palestina, Israel hakutakuwa na amani kamili.

Lakini hata hivyo, Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameelezea kuvunjwa moyo na hotuba iliyotolewa na John Kerry kuhusiana na jambo hilo, ambayo ameielezea kuwa haijakaa sawa.

Amesema ukweli ni kwamba Wapalestina wamekataa kukubali uwepo wa Israel.

Kwa upande wake, Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amesema atakuwa tayari kurudi katika mazungumzo pale tu Israel itakapoacha kujenga makaazi ya mapya ya wananchi wake katika eneo la Wapalestina.

Sikukuu ya krismas yaondoka na maisha ya watu.

Dar/Moshi. Watu kumi na moja wameripotiwa kufariki dunia katika matukio mbalimbali wakati wa Sikukuu ya Krimasi.Katika matukio hayo, watu watano wakiwamo wanafunzi wanne wamekufa maji jijini Dar es Salaam na Rombo, Kilimanjaro na wengine saba wameuawa na wananchi baada ya kuwatuhumu kukwapua vitu mbalimbali. Jijini Dar es Salaam, wanafunzi wawili moja wa shule ya msingi na mwingine sekondari, walikufa baada ya kuzama kwenye kina kirefu cha maji wakati wakiogelea. Naibu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya amesema watu hao walifariki dunia katika maeneo tofauti. Amesema mwanafunzi wa darasa la pili aliyekuwa anasoma Zanzibar, Hafidhi Bubu alikufa maji wakati akiogelea kwenye ufukwe wa Bamba Kigamboni. Mwanafunzi huyo alikuwa likizo kwa baba yake ndipo siku hiyo ya sikukuu alipokwenda kuogelea kwenye ufukwe huo. Siku hiyohiyo, mwanamume ambaye hajatambulika jina lake alifariki dunia baada ya kuzama kwenye kina kirefu wakati akiogelea katika eneo la Coco Beach.

Wezi wa meno ya Tembo ya sh.300 milioni wafungwa miaka 15

Morogoro. Mahakama ya Wilaya ya Morogoro imewahukumu watu watatu kifungo cha miaka 15 jela kila mmoja baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kupatikana na vipande 51 vya meno ya tembo vyenye thamani ya zaidi ya Sh300 milioni.

 Baada ya hukumu kusomwa wake na ndugu wa washtakiwa wameangua vilio hali iliyowafanya askari kuwaondoa na kuwapeleka nje ya jengo la Mahakama ili kuruhusu shughuli zingine kuendelea.

 Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Joyce Mkoi dhidi ya washtakiwa Abel Adrian na Anael Mkindi, wakazi wa Dar es Salaam na Erick Kyaruzi, mkazi wa Shinyanga.

 Mkoi amesema ameridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani na upande wa mashtaka ambao haukuacha shaka yoyote kwamba washtakiwa walitenda kosa hilo.

 Amesema biashara ya meno ya tembo inasababisha wanyama hao kuuawa hivyo kuikosesha Serikali mapato yatokanayo na utalii.

Kabla ya adhabu hiyo kutolewa, washtakiwa kwa nyakati tofauti waliiomba Mahakama iwapunguzie adhabu wakidai wana familia zinazowategemea.

 

Kyaruzi amedai mke wake ana umri mdogo na hilo ni kosa lake la kwanza. Upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Costantine Kakula uliiomba Mahakama kutoa adhabu kali dhidi ya washtakiwa kwa madai kuwa vitendo vya ujangili vimekithiri.

Washtakiwa walitenda kosa hilo Februari 8, 2012 eneo la Maseyu, Barabara ya Morogoro – Dar es Salaam.

 Ilidaiwa mahakamani kuwa idadi hiyo ya vipande vya meno hayo ni sawa na tembo 11 waliouawa.

 Ilidaiwa washtakiwa walikamatwa wakiwa na gari aina ya Toyota Land Cruiser lililobadilishwa namba ya usajili.

Upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi tisa katika kesi hiyo ambayo washtakiwa walijitetea wenyewe.

Simu ya Rais yatoa kelele za watu wakifanya mapenzi mahakamani

Rais Evo Morales akiwa mahakamani kwenye kikao pamoja na wanasheria wa kimataifa alianza kuchezea simu yake ambapo ghafla zilisikika sauti za watu wakifanya mapenzi kwenye simu yake. Bonyeza play hapa chini kutazama
bofya hapakuitazama

Utani wa Fid Q kwa AY baada ya kumpost mpenzi wake

Moja kati ya stori au post ambazo zimefuatilia sana leo December 27 2016 katika mitandao ya kijamii, ni pamoja na post za msanii wa Bongofleva Ambwene Yesaya ambaye wengi tunamfahamu kama AY kuamua kumpost mpenzi wake na kumtakia kheri ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa

Monday, 26 December 2016

Firmino akamatwa kwa kuendesha gari akiwa mlevi

Roberto Firmino wa Liverpool



Image caption Roberto Firmino wa Liverpool

Mchezaji wa Liverpool Roberto Firmino ameshtakiwa kwa kosa la kuendesha gari akiwa mlevi baada ya kukamatwa mkesha wa siku ya Krismasi.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alikamatwa baada ya gari lake kusimamishwa katikati mwa Liverpool mapema siku ya Jumamosi ,polisi wamesema.