Kiungo wa zamani wa Manchester United anatarajiwa kumrithi mkufunzi aaliyekuwa mkufunzi wa Swansea Bob Bradley, aliyetimuliwa usiku wa kuamkia leo na Klabu ya Swansea.
Awali, Giggs, mwenye umri wa miaka 43, alihojiwa mara mbili na timu hiyo kabla ya nafasi hiyo kuchukuliwa na Bradley mwezi Oktoba.
Bradley aliachishwa kazi baada ya kuiongoza Swansea kwa siku 85 pekee na kuiacha katika nafasi ya 19 kwenye ligi. Ingawa hana uzoefu mwingi, baada ya kustaafu, Giggs aliitumikia Manchester United chini ya David Moyes na kuwa naibu wa kocha, chini ya meneja wa zamani Louis van Gaal.
Nahodha huyo wa zamani wa Wales anadaiwa kufanya mazungumzo na wasimamizi wa Swansea, na mwenyekiti wa klabu hiyo, Huw Jenkins anadaiwa kuvutiwa na Giggs.
Naibu kocha wa Zamani wa United Rene Meulensteen, anaamini Giggs anatosha kuiongoza Swansea. "Siamini kuwa Giggs hana uzoefu, alipata ujuzi akiwa naibu mkufunzi chini ya Manchester United." Rene Aliiambia BBC Radio 5 Live.
Wengine wanaosakwa na klabu hiyo ni meneja wa Wales, Chris Coleman, mkufunzi wa zamani wa Leicester City Nigel Pearson na aliyekuwa mkufunzi wa Birmingham City manager Gary Rowett.
Hata hivyo, Mrithi wa Bradley anatarajiwa kuchukua usukani baada ya mechi yao ya nyumbani dhidi ya Bournemouth mwisho wa mwezi. Kwa sasa, timu hiyo inayoongozwa na wakufunzi wa muda Alan Curtis na Paul Williams watainoa timu hiyo hadi uteuzi utakapofanywa.
Swansea ilipoteza mechi yake ya saba kati ya mechi 11 kwa kupata kichapo cha 4-1 dhidi ya West Ham ikiongozwa na Bradley Timu hiyo ina alama 12 baada ya kukusanya pointi 8 pekee na kufungwa mabao 29.
No comments:
Post a Comment