Waziri Kerry amesema hatua hiyo ina nia ya kulinda uamuzi wa kuwepo kwa mataifa mawili ili kuzuia hatari ambayo ingeweza kutokea.
Amesema bila ya usalama wa Israel na uwepo wa Palestina, Israel hakutakuwa na amani kamili.
Lakini hata hivyo, Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameelezea kuvunjwa moyo na hotuba iliyotolewa na John Kerry kuhusiana na jambo hilo, ambayo ameielezea kuwa haijakaa sawa.
Amesema ukweli ni kwamba Wapalestina wamekataa kukubali uwepo wa Israel.
Kwa upande wake, Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amesema atakuwa tayari kurudi katika mazungumzo pale tu Israel itakapoacha kujenga makaazi ya mapya ya wananchi wake katika eneo la Wapalestina.
No comments:
Post a Comment