Taifa la Guinea-Bissau ndio taifa lililofaidika sana katika orodha mpya ya shirikisho la soka duniani Fifa mwaka 2016 baada ya kupanda nafasi 78 tangu Disemba mwaka uliopita.
Taifa hilo sasa limeorodheshwa la 68 katika orodha ya dunia na la 15 barani Afrika.
Hatua hiyo inamaanisha kwamba Guinea Bissau ipo juu ya mataifa ya Uganda ,Togo na Zimbabwe ambayo pia yamefuzu katika kombe la mataifa ya Afrika nchini Gabon.
Senegal inakamilisha mwaka huu ikiwa ndio taifa linaloongoza barani Afrika na nambari 33 duniani.
Guinea Bissau ilifuzu katika michuano ya mataifa ya Afrika baada ya kuishinda Kenya na Zambia mwaka 2016.
Walipoteza mechi yao ya mwisho dhidi ya Congo-Brazaville lakini ikafanikiwa kumaliza katika kilele cha jedwali ili kuweza kufuzu Gabon.
Katika orodha ya dunia Argentina bado inasalia katika nafasi ya kwanza.
Orodha ya mataifa ya Afrika duniani:
Senegal (33)
Ivory Coast (34)
Tunisia (35)
Egypt (36)
Algeria (38)
DR Congo(48)
Burkina Faso (50)
Nigeria (51) (hakufuzu Gabon 2017)
Ghana (53)
Morocco (57)
No comments:
Post a Comment